TETESI KATIKA SOKA LA ULAYA 09 OCT 2017
Manchester City wamekuwa na "mazungumzo mazito" kuhusu uwezekano wao kumnunua mshambuliaji wa Barcelona Lionel Messi, 30, kwa euro 400m(£358m) mwezi Januari. Mchezaji huyo wa Argentina bado hajatia saini mkataba mpya katika klabu hiyo ya La Liga. Barcelona wanamfuatilia kwa karibu mshambuliaji wa Manchester United kutoka Ufaransa Anthony Martial, 21. Klabu hiyo ya La Liga pia inafuatilia kwa karibu kiungo wa kati wa Tottenham Dele Alli, 21, kama mbadala baada yao kutatizika kumpata kiungo wa Liverpool Philippe Coutinho, 25 Mchezaji wa kimataifa wa zamani wa Italia Andrea Pirlo, 38, amekataa kukanusha taarifa kwamba huenda akajiunga na Antonio Conte kama mkufunzi Chelsea baada ya kutangaza kwamba atastaafu mwisho wa msimu wa MLS ambapo huchezea klabu ya New York City. Paris St-Germain wanammezea mate mlindalango wa Manchester United David de Gea, 26. Arsenal wanataka kumnunua kiungo wa kati Miguel Almiron, 23, kutoka Atlanta United ambaye anakadi...