JUPP HEYNCKES KOCHA MPYA WA BAYERN MUNICH
Bayern Munich imemuajiri aliyekuwa kocha wa zamani wa timu hiyo Jupp Heynckes kama kocha mpya Hadi mwisho wa msimu huu kutokana na kufukuzwa kazi kwa Carlo Ancelotti
Ancelotti aliondoka mwezi Septemba huku miamba hiyo ya Ujerumani ikiwa katika nafasi ya tatu ikiwa nyuma ya viongozi wa ligi Borussia Dortmund kwa alama tano.
Heynckes mwenye umri wa miaka 72 ameifunza Bayern mara tatu mwisho ikiwa 2013 wakati ambapo timu hiyo ilishinda kombe la vilabu bingwa, Bundelsiga na Kombe la Ujerumani kwa mara tatu.
''Ningependa kurudi katika klabu yoyote ilie duniani'', alisema.''Bayern Munich iko karibu na moyo wangu'' .
''Mimi na wafanyikazi wangu tutatumia kila njia ili kuleta tena ufanisi wa soka kwa mashabiki.Niko tayari kukabiliana na changamoto hiyo''.