TETESI KATIKA SOKA LA ULAYA 09 OCT 2017


Manchester City wamekuwa na "mazungumzo mazito" kuhusu uwezekano wao kumnunua mshambuliaji wa Barcelona Lionel Messi, 30, kwa euro 400m(£358m) mwezi Januari.
Mchezaji huyo wa Argentina bado hajatia saini mkataba mpya katika klabu hiyo ya La Liga.


Barcelona wanamfuatilia kwa karibu mshambuliaji wa Manchester United kutoka Ufaransa Anthony Martial, 21.
Klabu hiyo ya La Liga pia inafuatilia kwa karibu kiungo wa kati wa Tottenham Dele Alli, 21, kama mbadala baada yao kutatizika kumpata kiungo wa Liverpool Philippe Coutinho, 25
Mchezaji wa kimataifa wa zamani wa Italia Andrea Pirlo, 38, amekataa kukanusha taarifa kwamba huenda akajiunga na Antonio Conte kama mkufunzi Chelsea baada ya kutangaza kwamba atastaafu mwisho wa msimu wa MLS ambapo huchezea klabu ya New York City. 

Paris St-Germain wanammezea mate mlindalango wa Manchester United David de Gea, 26. 

Arsenal wanataka kumnunua kiungo wa kati Miguel Almiron, 23, kutoka Atlanta United ambaye anakadiriwa kuwa na thamani ya £18m. Mchezaji huyo wa taifa wa Paraguay alijiunga na klabu hiyo inayocheza ligi ya MLS miezi 10 iliyopita kwa £10m. 
Beki wa zamani wa Arsenal Bacary Sagna, 34, ambaye aliachiliwa na Manchester City majira ya joto bado hajapata klabu, na anahusishwa na kuhamia Leicester. 

Mshambuliaji aliye Swansea kwa mkopo Tammy Abraham, 20, anahitaji kufuata mfano wa Didier Drogba na Samuel Eto'o iwapo anataka kufanikiwa Chelsea, naibu mkufunzi mkuu wa klabu hiyo ya Wales Claude Makelele amesema. 
Arsene Wenger amemwambia Jack Wilshere, 25, kwamba ana hadi Desemba kuimarisha hali yake na kuthibitisha kwamba anaweza kuichezea klabu hiyo mara kwa mara. 

Benjamin Mendy, 23, wa Manchester City ametembelea kliniki moja Barcelona kufanyiwa uchunguzi anapoendelea kupata nafuu kwa miezi minne baada ya kuumia kwenye kano za goti. 
Mchezaji wa Manchester City Kevin De Bruyne, 26, amesema alikuwa na wasiwasi sana wa kuumia uwanjani Bosnia wakati wa mechi ambayo Ubelgiji walishinda Jumamosi. Amesema uwanja huo ndio mbaya zaidi ambao amechezea tangu akiwa na miaka saba.

Sir Alex Ferguson "alikataa fursa ya kumnunua Zinedine Zidane" kwa sababu alimpendelea zaidi Eric Cantona katika nafasi inayochezwa na wawili hao Manchester United, mwenyekiti wa zamani wa klabu hiyo Martin Edwards amesema. 
Mdosi wa zamani wa Newcastle Chris Hughton - ambaye kwa sasa ni mkufunzi mkuu Brighton - anaamini klabu hiyo inastahili kufanikiwa "chini ya mikono salama" ya Rafael Benitez.
AC Milan wanatarajiwa kuwasilisha dau ya £80m kutaka kumchukua mchezaji wa Manchester City Sergio Aguero, 29, Januari.

Matumaini ya kalbu hiyo ya Italia kumchukua Aguero huenda yakaimarishwa iwapo Manchester City watafanikiwa kwenye dau yao ya £20m kwa nyota wa Arsenal Alexis Sanchez, 28, kwenye dirisha ndogo la kuhama wachezaji Janauri. 
Arsenal wanmnyatia mshambuliaji wa Manchester United kutoka Ufaransa Anthony Martial, 21, ambapo wanataka ajaze nafasi itakayoachwa na Sanchez. 

Popular posts from this blog

LIST OF THE OLDEST UNIVERSITY IN AFRICA

ALIYEJIFANYA USALAMA WA TAIFA KUFIKISHWA MAHAKAMANI