TETESI ZA SOKA LA ULAYA JUMAPILI HII 17/12/2017
Jonny Evans.
Manchester United wanataka kumleta mlinzi Jonny Evans Old Trafford, miaka miwili unusu baada ya kumuuza mchezaji huyo wa miaka 29 kwenda West Brom, lakini Manchester City na Arsenal wanammezea mate.
Juventus wanaonekana kuwa na nia ya kumuuza mlinzi Alex Sandro lakini Chelsea walioshindwa kumsaini mbrazil huyo msimu huu, wanakabiliwa na ushindani kutoka Manchester City, Manchester United na Paris St-Germain.
Klopp.
Daniel Sturridge ameambiwa anaweza kuondoka Liverpool kwa mkopo mwezi ujao na meneja Jurgen Klopp wakati mchezaji huyo wa miaka 28 raia wa England anataka kujitafutia nafasi katika kombe la dunia .
Meneja wa Liverpool anasema kuwa alishinikizwa na maajenti wake kumsaini Mohamed Salah msimu huu baada ya hofu kuwa wing'a huyo wa Misri wa umri wa miaka 25 alikuwa mdogo sana kuweza kufanikiwa katika Premier League.
Mohamed Salah.
Manchester United wanatathmini ikiwa watatoa ofa ya karibu milioni 30 kwa wing'a wa Bordeaux mbrazil Malcom, 20, mwezi Januari.
Malcom
Manchester City wamemtazama mlinzi wa Augsburg mjerumani Philipp Max, 24, wakati wanataka kujaza nafasi ya mfaransa aliye na jeraha Benjamin Mendy.
Philipp max
Meneja wa Everton Sam Allardyce analenga kumsaini mshambuliaji wa Crystal Palace mBelgiji Christian Benteke, 27, wakati wa msimu mpya wa kusaini wachezaji wapya mwezi ujao.