TETESI ZA SOKA LA ULAYA LEO 06/10/2017
Arsenal itamuuza mshambuliaji wao Theo Walcot na kiungo wa kati Mesut Ozil wote wakiwa na umri wa miaka 28 mnamo mwezi Januari.
Walcott anatarajiwa kujiunga na klabu yake ya zamani Southampton.
Ozil anataka kuichezea Barcelona, Real Madrid ama Manchester United iwapo ataondoka Arsenal lakini anaweza kutia saini mkataba mpya.
Paris St-Germain inamtaka mshambuliaji wa Arsenal Alexis Sanchez, 28, wakati kandarasi yake itakapokamilika msimu ujao na kumuuza mshambuliaji Edison Cavani, 30.
Cavani ambaye ni raia wa Uruguay huenda akasajiliwa na Real Madrid mwezi Januari.
Geofrey Kondogbia.
Tottenham na Liverpool wote wanamtaka kiungo wa kati wa Inter Milan ,24, Geofrey Kondogbia ambaye yuko kwa mkopo katika klabu ya Valencia.
Kai Haverts.
Liverpool huenda wakamsajili kiungo wa kati wa Bayer Leverkusen Kai Haverts, 18, baada ya maskauti kumtazama akiifungia timu ya Ujerumani ya vijana wasiozidi umri wa miaka 19 mabao manne.
Beki wa Tottenham Toby Alderweireld ,28, amesema kuwa anafurahi kusalia katika klabu hiyo licha ya kutokamilisha kandarasi mpya na klabu hiyo ya ligi ya Premia.
Mauricio Pochettino.
Mkufunzi wa Spurs Mauricio Pochettino anataka kuwachezesha pamoja viungo wa kati Ross Barkley ,23, na Eric Dier, 23, iwapo atafanikiwa kumsajili kiungo huyo wa kati kutoka Everton mnamo mwezi Januari.
Kiungo wa kati wa Paris St-Germain Adrien Rabiot, 22, anasema kuwa angependa kucheza katika ligi ya Uingereza siku moja na amekuwa shabiki sugu wa Liverpool .
Oscar.
Mchezaji wa zamani wa Chelsea Oscar, 26, anasema kuwa yuko tayari kurudi katika klabu hiyo .
Raia huyo wa Brazil alijiunga na klabu ya China Shanghai SIPG mnamo mwezi January.
Mshambuliaji wa Brazil Lucas Moura, 25, ameshauriwa na mchezaji wa zamani wa Chelsea Alex kuondoka PSG na kujiunga na Arsenal.
Daley Blind
Fenerbahce huenda ikataka kumsajili beki wa Manchester United Daley Blind, 27.
Beki wa zamani wa Arsenal Thomas Vermaelen, 31, anasema kuwa Barcelona ilikataa kumwachilia ajiunge na Everton msimu uliopita
Mshambuliaji wa Burnley Chris Wood, 25, anasema kuwa hakukataa kuichezea Leeds United kabla ya uhamisho wake wa £18m kueleka Clarets.
Adrien Silva.
Mchezaji wa Leicester Adrien Silva, 28, amefanya mazoezi na klabu yake mpya kwa mara ya kwanza licha ya mchezaji huyo kutoruhusiwa kushiriki katika mechi kali hadi Januari.
Mkufunzi wa timu ya Uingereza ya wachezaji wasiozidi umri wa miaka 21 Aidy Boothroyd anasema kuwa wanakabiliwa na changamoto kubwa kutoka kwa Nigeria ya kumzuia mshambuliaji Tammy Abraham, 20, na Winga Sheyi Ojo,20.
Mshambuliaji Cristiano Ronaldo, 32, amemtaka rais wa Real Madrid Florentino Perez kumsajili kiungo wa kati wa Sporting Lisbon William Carvalho, 25.