DONALD NGOMA KUKAA NJE KWA WIKI MOJA

Mshambuliaji wa Yanga, Donald Ngoma atahitaji mapumziko ya wiki moja pekee kabla ya kuanza tena mazoezi baada ya kuumia Jumamosi iliyopita katika mchezo wa ligi kuu dhidi ya Mtibwa Sugar.
Katika mchezo huyo Ngoma aliondoka uwanjani dakika ya 77 akiwa anachechemea na nafasi yake kuchukuliwa na Juma Mahadhi huku Yanga ikilazimishwa sare ya 0-0.
Taarifa hiyo imetolewa na daktari wa Yanga, Edward Bavu baada ya jana kufanyiwa vipimo na kugundulika kuwa na matatizo kwenye misuli ya paja, jambo linalomfanya asiendelee na mazoezi kwa kipindi hicho.
Kikosi cha mabingwa hao watetezi wa ligi kuu kinaendelea kujifua katika dimba la Uhuru kujiandaa na mchezo wake dhidi ya Kagera utakaopigwa Jumamosi ya Oktoba 14 katika dimba la Kaitaba, Bukoba

Popular posts from this blog

LIST OF THE OLDEST UNIVERSITY IN AFRICA

LIST YA MIJI HATARI NCHINI MAREKANI

Top 7 Questions and Answers on Leadership