SERGIO AGUERO APATA AJALI


Mshambuliaji wa Manchester City Sergio Aguero amejeruhiwa katika ajali ya barabarani mjini Amsterdam, saa chache baada ya kuhudhuria tamasha.
Raia huyo wa Argentina, mwenye umri wa miaka 29, alikuwa ndani ya taxi akielekea katika uwanja wa ndege baada ya kuhudhuria tamasha la muimbaji Maluma.
City imesema "alikuwa Uholanzi katika siku yake ya mapumziko na amepata majeraha"
Aguero anatarajiwa kurudi Manchester Ijumaa hii na atakaguliwa na kikosi cha madaktari wa City kabla ya kuelekea kwa mchuano wa Premier League watakapokaribishwa na Chelsea Jumamosi.
Polisi Amsterdam wameithibitishia kwamba watu wawili walikuwa ndaniya taxi iliyohusika katika ajali katika eneo la De Boelelaan mjini humo.

Popular posts from this blog

LIST OF THE OLDEST UNIVERSITY IN AFRICA

ALIYEJIFANYA USALAMA WA TAIFA KUFIKISHWA MAHAKAMANI