RATIBA YA VPL KUPANGWA MPYA

Kaimu katibu mkuu wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Kidao Wilfred ameunda kikosi kazi cha wataalamu wanne wa shirikisho hilo kuangalia upya ratiba ya ligi kuu Tanzania Bara inayorushwa kupitia Azam TV.
Kidao ambaye ana siku tisa ofisini tangu ashike wadhifa huo, amesema lengo la uamuzi huo ni kuondoa kila aina ya kero inayoweza kuibuka katikati ya mashindano.
Amesema kikosi hicho kitakuwa na kazi ya kutengeneza ratiba mpya ili itakapotoka, isibadilike hadi mwisho wa msimu isipokuwa kwa mazingira yaliyo nje ya uwezo wa kibinadamu
Hatua hiyo inakuja baada ya kuwepo kwa malalamiko kutoka kwa wadau kutokana na kitendo cha ratiba ya ligi kuu msimu huu kupanguliwa ili kupisha mchezo wa Taifa Stars, ambapo Kidao amewaomba radhi wadau wote kwa dosari hiyo na kutangaza kuwachukulia hatua waliohusika.
Amesema hatua hizo za kinidhamu si kwa kupanga mechi wakati wa wiki ya FIFA pekee, bali maofisa hao wamehusika kupanga ratiba ambayo tathmini ya uongozi imeonesha kwamba si rafiki kwa timu zote 16 zinazoshiriki ligi hiyo.
Akianisha udhaifu mwingine wa ratiba hiyo, Kidao amesema kuna baadhi ya timu zimepangiwa kucheza mechi nyingi nyumbani au ugenini wakati wa kumaliza ligi hasa duru la pili linaloanzia Desemba, 2017 hadi Mei, 2018.
Ratiba hiyo ilipangwa kabla ya uongozi mpya wa TFF ulio chini ya rais Wallace Karia

Popular posts from this blog

LIST OF THE OLDEST UNIVERSITY IN AFRICA

LIST YA MIJI HATARI NCHINI MAREKANI

Top 7 Questions and Answers on Leadership