MECHI YA SIMBA NA HARD ROCK KUFANYIKA JUMAPILI
Mchezo wa kirafiki kati ya wekundu wa Msimbazi, Simba SC dhidi ya timu ya Hard Rock kutoka visiwani Pemba umesogezwa mbele na sasa utapigwa Jumapili ya Septemba 3.
Awali mchezo huo ulipangwa kupigwa leo Septemba Mosi katika dimba la Uhuru lakini imeamua kuusogeza mbele ili kuwapisha Botswana ambao leo wanautumia uwanja huo kwa ajili ya mazoezi yao ya mwisho kabla ya kuivaa Stars Jumamosi.
klabu ya Simba ambayo inajiandaa na mchezo wake wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Azam FC Septemba 6, imewaomba radhi mashibiki wa kandanda nchini kutokana na hatua hiyo.