KLABU YA BAYERN MUNICH YAMFUTA KAZI CARLO ANCELOTTI
Kufuatia kichapo cha 3-0 dhidi ya PSG , bodi ya klabu hiyo iliamua kumfuta kazi raia huyo wa Italy ambay alichukua mahala pake Pepe Guardiola msimu uliopita.
Ancelotti mwenye umri wa miaka 58, aliisaidia Bayern kushinda taji la Bundesliga, lakini hawakuweza kufika katika raundi ya muondoano ya kombe la vilabu bingwa pamoja na nusu fainali ya kombe la Ujerumani.
Naibu meneja Willy Sagnol ataiongoza klabu hiyo kwa muda.
Bayern wako katika nafasi ya tatu katika jedwali la ligi , wakiwa alama tatu nyuma ya Borussia Dortmund ,wakiwa wameshinda mara nne.