HUYU NDIYE MWAMUZI WA MECHI KATI TAIFA STARS NA BOTSWANA

Mwamuzi wa kimataifa, Elly Sasii ndiye mwamuzi aliyepangwa kuchezesha mchezo wa kirafiki kati ya Taifa Stars ya Tanzania na Zebras ‘Pundamilia’ ya Botswana utakaofanyika kesho Jumamosi Septemba 2 na kurushwa LIVE kupitia Azam Sports 2.
Katika mchezo huo wa kirafiki wa kimataifa utakaofanyika kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam waamuzi wasaidizi watakuwa Soud Lillah (Line 1) na Frank Komba (Line 2) wakati mwamuzi wa akiba (Forth Official) atakuwa Israel Nkongo.
Kocha mkuu wa Taifa Stars, Salum Mayanga leo amezungumza na wanahabari  na kuthibitisha kuwa kikosi chake kiko imara kwa mapambano.
Kwa upande wa Kocha wa Botswana, David Bright amesema yeye ni kocha mpya na amejitahidi kuteua timu mpya yenye mchanganyiko wa vijana na wazoefu aliokuja nao kuwajaribu kwa nyota wa Kitanzania.
Mchezo huo utaanza saa 10.00 jioni unaochezwa chini ya utaratibu wa kalenda ya FIFA ambapo TFF imepanga watazamaji waingie uwanjani kwa kiingilio cha shilingi 10,000 kwa jukwaa kuu na Sh 5,000 kwa mzunguko.

Popular posts from this blog

LIST OF THE OLDEST UNIVERSITY IN AFRICA

LIST YA MATAJIRI WAKUBWA DUNIANI

LIST YA MIJI HATARI NCHINI MAREKANI