BOTSWANA WATUA NCHINI KUMECHANA NA TAIFA STARS
Msafara wa timu ya taifa ya Botswana imetua nchini usiku wa kuamkia leo tayari kwa mechi ya kirafiki iliyo kwenye kalenda ya FIFA dhidi ya timu ya taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’, itakayopigwa kesho katika uwanja wa Uhuru na kurushwa mbashara kupitia Azam Sports 2.
Botswana inayonolewa na David Bright imekuja na kikosi cha wachezaji 18 ambacho kinafanya mazoezi katika uwanja wa Karume asubuhi ya leo.
wachezaji waliotua na kikosi hicho ni pamoja na makipa Mampule masule, Noah Maposa na Antony Gouws.
Walinzi ni Letsweletse, Mosha Gaolaolwe, Simisane Mathumo, Thabang Mosigi, Lesenya Ramorake, Tapiwa Gadibolae na Bokani Leeton.
Viungo ni Alphonse Modisaotsile, Maano Ditshupo, Katlego Masole, Gift Moyo, Segolame Boy, Lemponye Tshireletso, Thero Setsile, Kabelo Seakanyeng, Jackson, Lemogang maswena.
Washambuliaji ni Tumisang Orebonye, Jarome Ramathakwane, Tebogo Sembowa, Hendric Moyo na Boipelo Oaitse.