WOLPER ADAI ANAOGOPA KUTEMBEA NA WAUME ZA WATU

Malkia wa filamu bongo, Jacqueline Wolper amefunguka na kusema hawezi kutoka kimapenzi na wanaume ambao wameoa kwa madai anahofia wanaweza wakatelekeza familia zao kwa maana yeye akichukua kitu huwa hawi lelemama hata kidogo. Wolper amebainisha hayo wakati akipiga stori na mmoja wa watangazaji wa kipindi cha Planet Bongo ya East AFrica Radio, Big Chawa na kusema amekuwa muoga sana kufanya jambo hilo kwa kuwa anaogopa laana. "Nakuwa naogopa sana, nawaheshimu sana kwa sababu wengi wao wanakuwa ni waume za watu halafu hakuna laana mbaya kama kutembea na mume wa mtu, 'otherwise' ukute huyo mtu anasumbuliwa na mke wake unajua kuna wanawake ni wakorofi tu wanakuwa wanawasumbua waume zao na kupelekea kutafuta pumziko nje labda itokee hivyo lakini hivi hivi naona kama ni baba yangu", alisema Wolper. Pamoja na hayo, Wolper ameendela kwa kufafanua baadhi ya mambo kwa kusema "No siongelei umri hapa naongelea imani, kwa sababu mimi nikimchukua mume wa mtu sitokuwa lele mama halafu sasa kule nyumbani kwake atakuwa anapunguza mapenzi kwa hiyo kidogo nakuwa na huruma na ndiyo maana mimi nataka niwe na cha kwangu sitaki kuiba cha mtu". Katika siku za hivi karibuni Jacqueline Wolper amekuwa akiandamwa sana katika skendo la kutoka na wanaume wadogo kiumri japo yeye mwenyewe amekuwa mgumu kuweka bayana kuhusiana na mambo hayo ambayo wanazungumziwa mtaani.

Popular posts from this blog

LIST OF THE OLDEST UNIVERSITY IN AFRICA

LIST YA MIJI HATARI NCHINI MAREKANI

Top 7 Questions and Answers on Leadership