UJUMBE WA MESSI KWA NEYMAR
Lionel Messi ambaye amecheza na Neymar kwa miaka minne toka staa huyo ajiunge na Barcelona, ametumia ukurasa wake wa instagram kumtakia kila la kheri Neymar ambaye leo inaaminika ameshasafiri kuelekea Pariskukamilisha uhamisho huo.
“Ilikuwa ni heshima kushea chumba kimoja cha kubadilishia nguo na wewe kwa miaka yote hiyo rafiki yangu Neymar kila la kheri katika hatua mpya ya maisha yako
Hayo ni maneno ya messi.
Taarifa zilizopo kwa sasa katika mitandao ya kijamii duniani kote na vyombo vya habari vya Ulaya ni kuhusiana na ishu ya mshambuliaji wa kimataifa wa Brazil anayeichezea FC Barcelona Neymar kuhusishwa kukaribia kujiunga na Paris Saint Germain(PSG)ya Ufaransa.
Habari kutoka katika mitandao mingi ya Ulaya inaripoti kuwa PSG hadi sasa wana asilimia 90 ya kumpata Neymar kutokana na mchezaji huyo kuiomba na kuishinikiza Barcelona imuuze, baada ya kocha kumpa ruhusa Neymar na FC Barcelona kuthibitisha Neymar kuombwa kuuzwa.

