Uchaguzi mkuu Rwanda Paul Kagame Kaibuka mshindi
Tume ya Uchaguzi nchini Rwanda inasema kuwa Paul Kagame ameshinda uchaguzi wa uraisi uliyofanyika jana nchini humo.
Tume hiyo imesema matokeo ya awali yameonyesha kuwa Rais Kagame alishinda kwa asilimia 98 ya kura zilizohesabiwa. Rais Kagame ambaye amekuwa madarakani kwa miaka kumi na saba sasa atahudumu muhula wa tatu wa miaka saba.

Rais Kagame aliingia madarakani mwaka 1994 wakati kundi lake la waasi lilichukua udhibiti wa mji mkuu Kigali na kukomesha mauaji ya kimbart ambapo watu 800,000 watusi na wahutu wenye msimamo wa wastani waliuawa.
Katiba ya Rwanda ilifanyiwa mabadiliko mwaka 2015 na kumpa Kagame fursa ya kusalia madarakani hadi mwaka 2034