TOP 4 YA HANS POPPE

Mwenyekiti wa kamati ya usajili ya klabu ya Simba Zacharia Hans Poppe ametajatimu nne zitakazomaliza nafasi za juu ‘ top four’ msimu huu wa ligi kuu Tanzania bara unaotarajiwa kufunguliwa kwa mechi ya Ngao ya Jamii kati ya Simba na Yanga August 23, 2017. “Kwa utabiri wangu, naweza kusema kuna Simba, Yanga, Azam na Singida United ndio zinaweza kuingia kwenye top four lakini pia tutaona ligi itakapoanza. Kwa hizi mechi za kirafiki nilizoangalia, wenzetu wa Yanga kama wataendelea kucheza kama walivyocheza na Singida wanaweza wasifike top four kama huko mbele watachanganya na kufanya vizuri basi watakuwepo top four,” Hans Pope. “Timu kama Singida United imesajili kwa nguvu sana lakini napenda kuwaasa kama wamesajili hivyo kwa msingi wa kuchukua ubingwa kidogo itakuwa ngumu na wanaweza wakawa disappointed kwa sababu hawachezi kama timu na itawachukua muda wao kucheza kama timu na kupata uzoefu unaotakiwa.” “Nagemegea kuwaona wakifanya vizuri na wanaweza kuwepo kwenye top four lakini si dhani kama watakuwa katika nafasi ya kuchukua ubingwa.” Ikimbukwe kwamba, Hans Poppe ametaja top four yake kutokana na uzoefu wake wa soka kwenye ligi kuu Tanzania lakini hajataja timu ambayo itashinda ubingwa wa ligi kuu msimu huu.

Popular posts from this blog

LIST OF THE OLDEST UNIVERSITY IN AFRICA

LIST YA MIJI HATARI NCHINI MAREKANI

LIST YA MATAJIRI WAKUBWA DUNIANI