TAARIFA KUHUSU SOKA LA ULAYA
Manchester United wamepewa matumaini na Real Madrid ya kumsajili Gareth Bale, 28.
Manchester United watampa mkataba mpya beki wa kushoto Luke Shaw, 22, ili kuepuka asiondoke bure mwisho wa mkataba wake.
Chelsea wanakaribia kumsajili kiungo wa Leicester City Danny Drinkwater, 27, kwa pauni milioni 40 pamoja na Alex Oxlade-Chamberlain, 24 kutoka Arsenal.
Chelsea wanakaribia kumuuza mshambuliaji wake Diego Costa, 28, kwenda Atletico Madrid kwa pauni milioni 30.
Liverpool bado wanamtaka beki Virgil van Dijk, 26.
Liverpool wamethibitisha kufikia makubaliano ya kumsajili Naby Keita kutoka Red Bull Leipzig ifikapo Julai mosi 2018.
Liverpool wapo tayari kutumia pauni milioni 135 kuwasajili Virgil van Dijk na Thomas Lemar, baada ya kukamilisha usajili wa Naby Keita.
Mateo Kovacic ameonesha nia ya kutaka kujiunga na Liverpool na kuondoka Real Madrid.
Monaco wamekataa dau la pili kutoka Liverpool la kumtaka Thomas Lemar.
Swansea wanataka kumsajili kiungo wa Bayern Munich Renato Sanchez, 20.
Manchester City wanapanga kupanda dau jingine kumtaka mshambuliaji wa Arsenal Alexis Sanchez, 28.
Manchester City wanapanga kupanda dau jipya kumtaka beki wa kati wa West Brom Jonny Evans, 29, baada ya dau la pauni milioni 21 kutoka kwa Leicester kukataliwa.
Beki wa Manchester City Eliaquim Mangala, 26, huenda akajiunga na West Brom kama sehemu ya mkataba wa kumsajili Jonny Evans.
Meneja wa West Brom Tony Pulis anarejea Emirates na dau la pauni milioni 13 kumtaka beki Kieran Gibbs.
Tottenham huenda wakamkosa beki wa PSG Serge Aurier, 24, ambaye anataka kwenda Manchester United.
Sam Allardyce huenda akarejea Crystal Palace iwapo Frank de Boer atafukuzwa kazi.
Daktari wa timu ya taifa ya Brazil Michael Simoni amesema tatizo la mgongo la kiungo wa Liverpool Philippe Coutinho linasababishwa na msongo wa mawazo kuhusiana na hatma yake.
Mkuu wa Juventus Beppe Marotta amesema klabu yake itapanda dau jipya kumtaka kiungo wa Liverpool Emre Can, 23, mwezi Januari.