STARTIMES WAZINDUA BUNDASLIGA

Wakati msimu mpya wa ligi kuu Ujerumani ‘Bundesliga’ ukitarajia kuanza Ijumaa ijayo, StarTimes Tanzania wamezindua msimu mpya nchini Tanzania. StarTimes ndio kampuni pekee yenye haki za kuonesha mechi za Bundesliga ‘mubashara’ kupitia ving’amuzi vyao vya dish na antenar. Vice Prisident wa StarTimes Tanzania Bi. Zuhura Hanif amesema, wateja wao watapata fursa ya kuhuhudia live zaidi ya mechi 300 kwa gharama nafuu. Tunapenda kuwajulisha wateja wetu kwamba Startimes Tanzania tumepata haki za kurusha matangazo ya live ligi ya Bundesliga, hivyo wateja wetu wanayo nafasi ya kuangalia mechi zaidi ya 300 mubashara kwa gharama nafuu kupitia Startimes” – Startimes Vice President Ms Zuhura Hanif. “Pia tunawatangazia waandishi wa habari kwamba washiriki kwenye shindano la kuripoti habari za Bundesliga ambapo mshindi atapelekwa Ujerumani kuangalia mechi za Bundesliga.” “Tunayo furaha pia ya kuwajulisha kwamba wateja wetu wataweza kuangalia ligi mbalimbali kama Serie A, Ligue 1, Belgium Pro League, EPL na michuano inayosimamiwa na FIFA kwa mwaka 2017 na 2018 ikiwemo World Cup.” Shaffih Dauda ambaye mwaka 2015 alikwenda Ujerumani na kushuhudia mechi kadhaa za Bundesliga amesema, uongozi wa Bundesliga unapambana kuhakikisha ligi yao inaonekana Afrika kupitia TV. Mwaka 2015 nilipata nafasi ya kutembelea makao makuu ya Bundesliga ndani ya Frankfurt. Uongozi wa Bundesliga una mipango madhubuti ya kuileta ligi hii barani Africa kupitia TV na zaidi ya hapo. Hatua ya msingi na ya kwanza ni kuleta ushirikiano na kampuni ya StartimesTz ili wakazi wa Africa wapate nafasi ya kuangalia kwa gharama nafuu,” Shaffih Dauda. Kwa upande wa afisa uhusiano na masoko wa Startimes Juma Suluhu amesema wamekuja na njia rahisi na nafuu kwa wateja wao kulipia ving’amuzi ambayo itawafanya wafurahie kuchagua king’amuzi chao. Tumeanzisha njia mpya ya malipo, sio lazima ulipie mwezi kwa mwezi. Unaweza kulipia kipindi cha siku kadhaa ambazo zina mechi zinaonyeshwa kupitia Startimes. Startimes ina lengo la kufanya kila mtu aangalie mechi live bila gharama kubwa,” Marketing and PR Officer – Juma Suluhu. “Tumeongeza idadi ya mechi za live kupitia king’amuzi chetu, kuanzia ligi ya Ubelgiji ambayo watanzania tunaifatilia kutokana na mchezaji wetu Samatta kucheza kule. Baadhi ya mechi za EPL, ligi yote ya Bundesliga, Ligue 1 ambayo ina Neymar, baadhi ya michezo ya NBA, mashindano ya kufunzu kombe la dunia na kombe la dunia lenyewe. Pia ukitazama gharama ya kulipia Startimes na mechi za live unazoangalia, unapata zaidi ya thamani unayolipia.”

Popular posts from this blog

LIST OF THE OLDEST UNIVERSITY IN AFRICA

LIST YA MIJI HATARI NCHINI MAREKANI

Top 7 Questions and Answers on Leadership