Maafisa kilimo mkoani Lindi wapatiwa Mafunzo

Mwezeshaji kutoka Jukwaa la Bioteknolojia Tanzania (OFAB), Dk.Emmarold Mneney (kulia), akitoa mafunzo ya siku moja ya kilimo chenye tija kwa maofisa Ugani wa Mkoa wa Lindi kwenye Maonyesho ya Kitaifa ya Nanenane yanayoendelea kwenye viwanja vya Ngongo mkoani Lindi.

Ofisa Kilimo kutoka Manispaa ya Lindi, Amina Pemba akizungumza kwenye mafunzo hayo.

Maofisa Ugani wakipata mafunzo

Ofisa Kilimo kutoka Manispaa ya Lindi, Hussein Mwapili, akitoa shukrani kwa niaba ya wenzake baada ya kupata mafunzo hayo

Mratibu wa Jukwaa la Bioteknolojia kwa Maendeleo ya Kilimo (OFAB), Philbert Nyinondi ambaye ni Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Kilimo Morogoro (SUA), akizungumza na maofisa ugani hao katika mafunzo hayo.

Wahamasishaji wa matumzi ya Bioteknolojia katika kilimo wakijadiliana wakati wa mafunzo hayo. Kulia ni Happiness John na Flaviana Anthony.