MATOKEO YA EUROPA LEAGUE

Everton walikuwa nyumbani Goodison Park kuikaribisha Hajduk Split na mabao mawili kutoka kwa mlinzi Michael Keane na Idrisa Gueye yaliifanya Everton kuibuka kidede kwa bao 2 kwa nunge. Ac Millan walishusha kipigo cha mbwa mwizi kwa KF Shkendija baada ya kuwapiga sita sifuri kwa mabao ya Andre Silva na Ricardo Montolivo waliofunga mara mbilimbili huku Fabio Borini na Luca Antoneli wakifunga mengine. Athletic Bilbao wakiwa ugenini waliifunga Phanathaikos bao 3 kwa 2 huku Wafaransa Marseille walifanikiwa kulazimisha sare ugenini ya bao moja kwa moja na Domzaie. Ajax wakiwa katika uwanja wao wa Amsterdam Arena walikubali kipigo cha bao moja kwa sifuri kutoka kwa Rosenrburg huku Fk Skobje wakiibamiza Fernabache mabao 2 kwa nunge.

Popular posts from this blog

LIST OF THE OLDEST UNIVERSITY IN AFRICA

LIST YA MIJI HATARI NCHINI MAREKANI

Top 7 Questions and Answers on Leadership