
Bado haieleweki na kila siku kunatokea habari mpya, juzi Costa alimponda Antinio Conte kwamba hawezi kuishi na wachezaji, jana Chelsea wakamtaka mchezaji huyo arudi kujiunga na klabu hiyo.
Lakini hii leo mapya yameibuka na sasa mshambuliaji huyo ametoa maamuzi yake ya wapi atacheza msimu ujao wa ligi na kusisitiza kwamba tayari ameshafanya maamuzi.
Diego Costa amesema yeye hawezi kurudi tena Uingereza na anarejea nyumbani Hispania kujiunga na klabu yake ya zamani ya Athletico Madrid ambayo ndiyo ilimuuza kwenda Chelsea.
“Nimeshafanya maamuzi yangu na ni lazima nirudi Athletico Madrid msimu ujao, hata kama Chelsea hawataki kuniachia lakini naamini suala langu litakamilika hivi karibuni na nitarejea Hispania” alisema Costa.
Diego Costa na Nemanja Matic walipewa muda wa kukamilisha usajili wao lakini Matic hadi sasa ndiye ameshapata timu huku Costa bado akiendelea kusubiria.
Wakati Costa akisema harudi Chelsea inasemekana Antonio Conte anataka kumsajili Andrea Belotti lakini tajiri kwa klabu hiyo Roman Abromovich hayupo tayari kutoa £100m kumnunua Belloti.