BEN POL ADAI ATAKI TENA MASWALI KUHUSU MAMBO YAKE BINAFSI



Msanii wa RnB Bongo, Ben Pol ameweka wazi kuwa kwa sasa hapendi kuulizwa maswali kuhusu Ebitoke, mtoto na mahusiano.
Muimbaji huyo amesema kutokana na kazi zake ambazo anataka kuzifanya kwa sasa inamlazimu kufanya hivyo.
“Kwa series ya kazi zangu zinazokuja ningependa sana vitu binafsi nisiviongelee zaidi au hadi pale nitakapokuwa tayari kuzungumzia Ben Pol anafanya nini sasa hivi nianze kuzungumzia,”

Ameongeza kuwa, “kwa hiyo sipo comfortable sana kusema vitu binafsi mahusiano, sijui mtoto nataka kupunguza kuvizungumzia hivyo vitu kwa sasa hivi kusema kweli,” amesisitiza.

Ben Pol ambaye anadai kuwa katika uhusiano wa kimapenzi na mchekeshaji Ebitoke amebainisha hilo ili kufanya uhusiano wao kuwa binafsi zaidi.

Popular posts from this blog

LIST OF THE OLDEST UNIVERSITY IN AFRICA

LIST YA MATAJIRI WAKUBWA DUNIANI

LIST YA MIJI HATARI NCHINI MAREKANI