AWAMU YA PILI YA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA MASOMO YA KIDATO CHA TANO HII HAPA

TAARIFA KWA UMMA Ofisi ya Rais – TAMISEMI inapenda kuwajulisha wananchi juu Orodha ya Wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na Kidato cha Tano kwa Awamu ya Pili kwa mwaka 2017. Wanafunzi hawa wataanza muhula wa kwanza wa masomo tarehe 24 Agosti, 2017 na hakutakuwa na mabadiliko yoyote ya shule. Wanafunzi wote wanatakiwa kuripoti katika shule walizopangwa kwa wakati. Endapo mwanafunzi atachelewa kuripoti hadi tarehe 08 Septemba 2017 ambayo ndiyo siku ya mwisho ya kuripoti, atakuwa amepoteza nafasi. Mwanafunzi mara uonapo jina lako kwenye tovuti ya Ofisi ya Rais – TAMISEMI kwamba umechaguliwa kujiunga na Kidato cha Tano, inabidi ku-download fomu ya kujiunga na shule husika kwenye mtandao. Orodha ya wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na Kidato cha Tano na Vyuo vya Ufundi awamu ya pili mwaka mwaka 2017 pamoja na fomu za kujiunga na shule (joining instructions) inapatikana kwenye tovuti ya Ofisi ya Rais-TAMISEMI ya www.tamisemi.go.tz Imetolewa na Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais –TAMISEMI 23 Agosti, 2017

Popular posts from this blog

LIST OF THE OLDEST UNIVERSITY IN AFRICA

LIST YA MATAJIRI WAKUBWA DUNIANI

LIST YA MIJI HATARI NCHINI MAREKANI