TETESI ZA SOKA LA ULAYA JUMAPILI HII 17/12/2017
Jonny Evans. Manchester United wanataka kumleta mlinzi Jonny Evans Old Trafford, miaka miwili unusu baada ya kumuuza mchezaji huyo wa miaka 29 kwenda West Brom, lakini Manchester City na Arsenal wanammezea mate. Juventus wanaonekana kuwa na nia ya kumuuza mlinzi Alex Sandro lakini Chelsea walioshindwa kumsaini mbrazil huyo msimu huu, wanakabiliwa na ushindani kutoka Manchester City, Manchester United na Paris St-Germain. Klopp. Daniel Sturridge ameambiwa anaweza kuondoka Liverpool kwa mkopo mwezi ujao na meneja Jurgen Klopp wakati mchezaji huyo wa miaka 28 raia wa England anataka kujitafutia nafasi katika kombe la dunia . Meneja wa Liverpool anasema kuwa alishinikizwa na maajenti wake kumsaini Mohamed Salah msimu huu baada ya hofu kuwa wing'a huyo...